TET KUADHIMISHA MIAKA 50, MEI 2025

Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) inatarajia kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ifikapo Mwezi Mei 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameeleza hilo  katika hafla ya uzinduzi wa usambazaji wa vitabu vya washindi wa tuzo ya Taifa ya Uandishi Bunifu iliyofanyika Novemba 18,2024 katika ofisi za TET Jijini Dar es Salaam. 

Dkt. Komba alisema kuwa,  katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50, TET inatarajia kufanya  shughuli mbalimbali za kielimu pamoja na za kijamii ikiwemo Kongamano la elimu na matembezi ya hisani.

"Kuelekea miaka hamsini  tumejipanga kufanya shughuli  kadhaa ambazo zitahusisha kazi zetu katika jamii " alisema Dkt.Komba .

Alisema, tukio hilo litawajumuisha wadau wa Elimu nchini watakaojadili masuala ya Elimu, mafunzo ya walimu kazini, upandaji wa miti kwa ajili ya kutunza mazingira  pamoja na matembezi  ya hisani ili kupata pesa za kuandaa vitabu kwaajili ya wanafunzi viziwi.

Aidha Dkt. Komba, aliomba wadau wa elimu kuwaunga mkono katika kuelekea kilele cha miaka 50 ya TET.

0/Post a Comment/Comments