Kampuni ya Mawasiliano, TIGO Tanzania katika kuelekea kufunga mwaka, wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha Sinza maalumu kilichopo jijini dar es salaam chenye watoto zaidi ya 93.
Akizungumiza mara baada ya kutoka msaada huo Mkurugenzi wa Tigo Dar es salaam, Bw. Aidan Komba amesema kama TIGO Tanzania wanatambua umuhimu wa watu wenye mahitaji maalumu na kuona kunaulazima wa kurejesha Kwa jamii faida wanayoipata.
" Kwa kweli msaada huu utawasaudia watoto kujimudu katika kufanya kazi zao za Kila siku kwani tumepata vifaa vya usafi, vitawasaidia watoto katika kufanya usafi hapa shuleni na vifaa vya cherehani vitawasaidia katika mafunzo ya ufundi" alisema
Kampuni ya TIGO Tanzania katika kuendeleza kurudisha Kwa jamii , itaendelea kutoka huduma hizo Kwa Kanda zote tisa nchini ambapo Leo wameanza kwenye Kanda hii ya Dar es salaam.
Tigo Tanzania imekuwa mstari mbele katika Kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihimiza watanzania kupendana na kushirikiana kwani Tanzania ni nchi yetu sote
Post a Comment