Kampuni ya mawasiliano, Tigo kupitia ofisi yake ya wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa kituo cha kulea watoto wenye mazingira magumu cha Raya Islamic Foundation. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kurudisha kwa jamii kutokana na faida wanayoipata.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Tigo-Pwani na Mashariki (Tanga na Morogoro), Abdully Ally, alisema kwamba zawadi hizo ni sehemu ya dhamira ya kampuni ya Tigo kushirikiana na jamii inayowazunguka ili kuimarisha maisha ya wale walio na uhitaji mkubwa.
Mifuko 5 ya sukari (kg 25 kila mmoja)mifuko 8 ya mchele (kg 25 kila mmoja),mifuko 20 ya sabuni ya unga,mifuko 10 ya unga wa mahindi (kg 25 kila mmoja),ndoo 5 za mafuta ya kupikia (lita 20 kila moja),mifuko 5 ya unga wa ngano,mifuko 4 ya maharage (kg 25 kila mmoja),dazeni 1 ya chumvi,katoni 3 za sabuni ya mche na bidhaa nyinginezo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo hicho, Bi. Raya Maganga aliishukuru kampuni ya Tigo kwa moyo wa ukarimu na akasisitiza kuwa kutoa kwa wenye uhitaji ni njia ya kujitengenezea akiba ya fadhila,"Wakati wa matatizo, utapata wa kujitoa kwako kama ulivyowahi kuwasaidia wengine," alisema.
Watoto wanaolelewa katika kituo hicho pia walitoa shukrani zao kwa Tigo na kuwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kutoa msaada wa aina hiyo, wakisisitiza kuwa msaada kama huo huwapa faraja na matumaini makubwa.
Hii ni hatua muhimu inayoonesha jinsi taasisi binafsi zinavyoweza kushiriki katika kuboresha maisha ya jamii kwa vitendo.
Post a Comment