Na Mwandishi Wetu.
Wateja wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo waliojishindia zawadi mbalimbali kwenye droo ya kwanza ya kampeni mpya ya Magift ya Kugift leo wamekabidhiwa zawadi zao, Wananchi hao wamekabidhiwa zawadi hizo kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo, jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza kwenye hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema;
“Kama ilivyo kawaida yetu, Tigo tunapenda kuweka furaha kwenye nyuso za wateja wetu, hivyo basi tumekuja tena na kampeni iitwayo Magift ya Kugift ambapo wiki hii tumefanya droo ya kwanza ya kutafuta washindi na tumepata jumla ya washindi 42, waliojishindia simu janja, washindi saba waliojishindia shilingi milioni moja kila mmoja na mshindi mmoja amejishindia shilingi milioni tano”.
Amesema kwa wafanyabiashara wao walijishindia zawadi hizo kwa kupokea malipo ya bidhaa wanazouza kutumia huduma Lipa kwa simu ya Tigo kutoka mitandao mbalimbali.
Kwa upande wa mawakala wao kigezo ilikuwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa pesa hivyo kuingia kwenye droo hiyo.
Meneja huyo alimalizia kwa kusema kampeni hiyo bado inaendelea na ndiyo kwanza imeanza bado kuna wiki zingine 12 kuelekea kampeni hiyo na kuwataka wananchini kuchangamkia kampeni hiyo kwa kufanya miamala kwa kutumia Tigo Pesa ili nao waweze kuingia kwenye droo ya ushindi huo. Alimaliza kusema Mary.
Kwa upande wa Wateja washindi wa shilingi milioni moja waliofika kwenye hafla hiyo kuchukua zawadi zao ni Adrian Milandu, Issa Masoud, Saadie Mwinyi, Zena Chiputa na Hilda Mavaga.
Kwa Wafanyabiashara waliojishindia shilingi milioni moja kila mmoja kwa kutumia huduma ya Lipa namba ya Tigo Pesa ni Mwanaidi Mbasi na Rose Mosha. Washindi wa shilingi milioni moja kila mmoja waliopo mikoani ni Mussa Nuhu wa Kagera na Kelvin Rwamugila aliyeko Dodoma.
Na mshindi wa pekee aliyeibuka na shilingi milioni tano katika droo hii ya kwanza ni Daud Eugen mkazi wa Salasala, Dar…
Post a Comment