********
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini
(TIRA) inatarajia kutoa taarifa ya utendaji wa soko la bima nchini kwa mwaka
2023.
Taarifa hiyo itatolewa Novemba 22, mwaka huu
katika hafla itakayofanyika kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki, Jijini Dar es
Salaam.
Kamishna wa TIRA, Dkt. Baghayo
Saqware, amesema kuwa soko la bima nchini limeonyesha ukuaji mzuri, ambapo
thamani ya soko imeongezeka kutoka shilingi trilioni 1.1 mwaka 2023 hadi
trilioni 1.2 mwaka huu, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa
uchumi wa nchi.
Ukuaji huu unahusishwa na mazingira
mazuri ya uwekezaji yaliyoanzishwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Saqware amesisitiza umuhimu wa
bima katika jamii, akieleza kwamba bima hutoa kinga kwa mali, afya, na
uwekezaji, na kwamba hutoa fidia wakati wa majanga ya kiuchumi na kijamii.
Aidha, ameelezea kwamba TIRA
inatumia mifumo ya kidigitali katika kuendesha soko la bima.
Pia, Kamishna Saqware amewahimiza
wananchi kuwa na utamaduni wa kutumia huduma ya bima ya nyumba, ambayo ni nafuu
na itasaidia katika kukabiliana na majanga kama vile moto.
Amefafanua kuwa bima ya nyumba ni bei ndogo na inaweza kugharimu chini ya asilimia moja ya thamani ya nyumba.
Post a Comment