Na Tausi Mbowe
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Kanda ya Ziwa Mashariki imefanya mafunzo ya kuwajengea uwezo watoa huduma katika sekta ya afya.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Novemba 13, 2024 jijini Mwanza.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Meneja wa Kanda ya Ziwa, Sophia Mziray ambako pamoja na mambo mengine alisisitiza umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za kuhifadhi matumizi na utunzaji wa kumbukumbu wa matumizi wa dawa hizo.
Aidha Mziray alisema kuwa kutofuata taratibu za matumizi ya dawa hizo kunaweza kusababisha madhara makubwa kwa wagonjwa , hivyo kuwataka wafamasia kuhakikisha wanafuata miongozo na taratibu zilizowekwa.
Mziray pia aliwataka wafamasia hao kurekebisha haraka mapungufu yaliyobainika wakati TMDA inapofanya kaguzi zake za mara kwa mara katika vituo vya afya na hospitali zilizoidhinishwa kununua na kutumia dawa hizo.
Meneja huyo alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja katika kusimamia na kutumia dawa ndani ya vituo vya afya.
Hata hivyo, Mziray ameeleza wasiwasi wake kuhusu ushiikiano kati ya wafamasia wauguzi na madaktari ambao ua
naweza kuathiri utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Akizungumzia sheria ya matumizi ya dawa za kulevya, Inspeta Wamba Msafiri Kamishna Msaidizi wa operationi kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya (DCEA), katika ofisi ya Ukanda wa Ziwa amesema chini ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2015 kifungu 9, ni kosa la jinai kwa yeyote anayekiuka matumizi ya dawa hizo na adhabu kali itachukuliwa dhidi yao.
Inspekta Msafiri aliwataka wananchi kuacha mara moja matumizi ya dawa hizo na kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo pindi wanapoona kuna uvunjwaji wa sheria.
Post a Comment