*******
Tozo zinazokatwa kwa watumiaji wa mafuta ya Petrol na Dizel imewezesha Mfuko wa Taifa wa Maji kutekeleza miradi ya maji ya zaidi ya Sh5 bilioni.
Hivi karibuni Bunge la Jamuhuri ya Muungano lilipitisha sheria ya kukata Sh50 katika kila lita ya mafuta ya Petrol na Dizel ili fesha hizo zitumike kwa ajili ya kusukuma maendeleo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Wakili Haji Nandule alisena hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu, zaidi ya Sh5 bilioni zilizokusanywa kutokana na mpango huo zilitolewa kama mkopo katka mamlaka za maji mijini na vijijini ili kutekeleza miradi ya maji.
"Matokeo yanaonekana fesha zinazokusanywa Inaenda kuteleleza miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo yanashida.' alisisitiza Afisa Mtendaji Mkuu huyo.
Nandule alisema uanzishwaji wa mfuko unalenga kuwa na uwepo wa chanzo cha fedha cha uhakika cha kutekeleza miradi kwa kukopesha mamla za maji za mijini na vijijini jambo linalofanywa kwa ufanisi mkubwa.
Alisema mpaka sasa Mfuko huo wenye watumishi 24 pekee unatoa mikopo kwa Mamlaka za maji mijini na Vijijini ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maji na kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji nchini.
Mtendaji huyo alizishukuru mamlaka hizo kwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati jambo linalichangia miradi hiyo kujengwa kwa haraka zaidi.
Post a Comment