WATENNDAJI WAKUU BORA 100 WATUNUKIWA TUZO KWA KUFANYA VIZURI


.............................

Na Mwandishi wetu- Dar es salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Sharif Ali Sharif amewataka vijana wa Kitanzania kubuni miradi inayoendana na sera za uwekezaji katika nchi ili waweze kuwa sehemu ya kujenga uchumi wa nchi yao kwa vitendo.

Akizumnguza Novemba 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Watendaji wakuu Bora 100 wa mwaka pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali zikiwemo kampuni zilizofanya vizuri mwaka 2024 Waziri Ali Sharif amesema vijana wana nafasi ya kufanya kampuni zao kutambulika katika soko la ndani na nje iwapo watatumia vyema mazingira mazuri ya uwekezaji ndani ya nchi yao.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Eastern Star Bw. Deogratius Kilawe ambaye ndie muandaaji wa  tuzo hizo kwa  ushirikiano wa Kampuni ya The Global CEO Institute amesema dhumuni la kuandaa Tuzo hizo ni  kusherehekea uongozi bora, kukuza uvumbuzi, na kuhamasisha kizazi kijacho cha watendaji pia kukuza na  kuweka viwango pamoja na kuleta mabadiliko chanya na matokeo ya kudumu katika tasnia na jumuiya tunazohudumia. 

Bw. Kilawe ameongeza kuwa ugawaji wa tuzo hizo umezingatia ubora wa kazi zilizofanywa na washiriki huku baadhi ya washindi wakisema tuzo hizo zinatia chachu kwa Kampuni za Kitanzania kuendelea kufanya vizuri mwaka hadi mwaka kwa kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la Kimataifa.

0/Post a Comment/Comments