Bei ya Mafuta Yashuka Desemba 2024, Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa Kupungua

.,..............

Bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa Imeendelea kushuka kwa mwezi Desemba mwaka huu.

Taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kushuka kwa bei hizo, licha ya gharama za uagizaji mafuta (Premiums) kuongezeka kwa wastani wa asilimia 7.26 kwa petroli na kupungua kwa asilimia 12.80 kwa dizeli na wastani wa asilimia 7.10 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, hakuna mabadiliko katika Bandari ya Tanga huku gharama zikiongezeka kwa wastani wa asilimia 15.67 kwa mafuta ya petroli na hakuna mabadiliko kwa mafuta ya dizeli katika Bandari ya Mtwara.

Kutokana na hilo, taarifa ya Ewura iliyotolewa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 inaonyesha kuwa bei ya rejareja ya mafuta ya petroli yanayopitia Bandari ya Dar es Salaam yameshuka kwa asilimia 1.55, dizeli ikishuka kwa asilimia 2.3 na mafuta ya taa kwa asilimia 3.9.

0/Post a Comment/Comments