Picha ya pamoja ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) wakiwa na Watendaji wa TASAC pamoja na Watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA ) katika Bandari ya Mbamba Bay.
***********
Watoa shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa
fedha ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay.
Na Mwandishi Wetu,Nyasa
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Meli
Tanzania (TASAC) limesema kuwa Bandari
ya Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma
ni Muhinu katika Maendeleo ya Kiuchumi.
Bandari hiyo itafungua biashara katika nchi za Malawi
,Zambia pamoja na Msumbiji katika
usafirishaji wa mizigo ya makaa ya mawe pamoja na mazao katika mikoa inayoizunguka ziwa hilo.
Akizungumza
katika ziara ya Bodi hiyo katika Bandari ya Mbamba Bay Mwenyekiti wa
Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia amesema
kuwa serikali imewekeza zaidi ya sh.bilioni 80 ambapo ujenzi wa Bandari hiyo
unatarajiwa kukamilika 2026.
Amesema kuwa fedha hizo zimetolewa na Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa kujengwa kwa bandari ya kisasa katika
Bandari ya Mbamba Bay.
Amesema kuwa bandari hiyo itakuwa na huduma zote ikiwa
TASAC wadhibiti na wasimamizi vyombo vya Usafiri majini kuhakikisha usalama
unazingatiwa.
Nah.Mandia amesema bandari hiyo zamani ilikuwa
changamoto ya Barabara lakini suala hilo serikali ilishakamilisha kwa asilimia
100.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Nelson Mlali amesema
hatua nzuri kwa ujenzi wa bandari kutokana na kuwepo miundombinu barabara hadi
bandarini.
Amesema kuwa bandari hiyo ipo katika eneo sahihi
katika kuchochea fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Nyasa pamoja nchi jirani
kutumia katika kusafirisha mizigo kwa kutumia bandari hiyo.
Mhandisi Mkuu Bandari za Ziwa Nyasa Fabian Paul
anaeleza hatua zilizofikiwa kwenye mradi huo wa mikakati kwa nchi.
Amesema kuwa ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia
tisa na kufikia hapo kulitokana kuchelewa kwa vifaa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri amesema bandari
hiyo inafungua milango kwa wawekezaji wa sekta mbalimbali huku wananchi wa
Wilaya ya Nyasa wakiamini kuwa kukamilika kwa bandari hiyo kwao ni fursa.
Mhandisi wa Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay Rafiki Joseph akitoa maelezo kwa Bodi ya Wakurugenzi wa TASAC wakati ilipotembelea Bandari hiyo.
Mhandisi Mkuu Bandari za Ziwa Nyasa wa TPA Fabian Paul akitoa maelezo kwa Bodi ya Wakurugenzi wa TASAC wakati ilipotembelea Bandari ya Mbamba Bay.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nah.Mussa Mandia akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri wakati Bodi hiyo ilipotembelea Ofisi hiyo kwa ajili ya ziara ya Bandari ya Mbamba Bay iliyopo Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.
Post a Comment