Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua mfumo wa kidigitali
utakaomuwezesha mtumiaji wa huduma za kifedha kuwasilisha malalamiko, kuanzia
Januari mwaka 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Ustawi wa Huduma Jumuishi
za Kifedha, BoT, Bi. Nangi Massawe amesema.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, Desemba 10, 2024, wakati akifungua warsha
ya siku mbili kuhusu mfumo wa malalamiko kwa wawakilishi wa taasisi za fedha
jijini Dar es Salaam.
“Mfumo umetengenezwa na kukamilika tunaamini ifikapo Januari katikati,
tutauzindua rasmi ili wananchi waweze kutuma malalamiko yao, ni muhimu sana kwa
kupitia warsha hii tuhakikishe wote tumeuelewa vizuri na kuanza kuutumia kabla
ya kuuzindua.” Amefafanua.
Naye Kaimu Meneja Idara ya Ulinzi wa Watumiaji wa Fedha, (Financial Consumer
Protection), Dkt. Khadija Kishimba, amesema BoT imeandaa warsha hiyo kwa
taasisi za fedha ili kuuelewa mfumo kwani wao ndio wanaokutana na (walaji)
wateja.
“Tubebe huu mfumo kwa sababu tunakwenda kusogeza huduma kwa wnanachi, tunataka
mwananchi alalamike kupitia kiganja chake, alalamike kupitia computer yake.”
Amesisitiza.
Amesema, “Ninyi ndio wenye mfumo, nasema hivyo kwasababu ninyi ndio mnaokutana
na wananchi, BoT imeandaa mfumo na tunapopeleka automation kwenye taasisi za
fedha sio lengo la BoT kubaki na mfumo huo, lengo letu wananchi watumie ili na
sisi tupate mrejesho.”
BoT YAJA NA MFUMO WA MALALAMIKO WA KIDIGITALI
******
Post a Comment