TAHADHARI NYOKA AINA YA CHATU UDSM



............

Na Mwandishi Wetu

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetoa tahadhari kuhusu nyoka aina ya chatu anayeonekana katika maeneo ya Shule ya Msingi Mlimani.

Kupitia taarifa iliyotolewa juzi na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala), Prof. Bernadeta Killian, alisema: “Napenda kutaarifu Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa kuna nyoka aina ya chatu ameonekana katika maeneo ya Shule ya Msingi Mlimani. Chatu huyo ana tabia ya kujificha kwenye majani na vichakani, hivyo si rahisi kumwona kwa wakati.”

Aidha, taarifa hiyo imesisitiza kuwa wanajumuiya wa chuo wachukue tahadhari kuhusu uwepo wa chatu huyo, wakati jitihada za kumtafuta zikiendelea.


0/Post a Comment/Comments