]
*******DKt. Biteko amemsema hayo leo Disemba 2, 2024 wakati akimwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua
Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na maonesho linaloendelea
Jijini Dar es Salaam.
Amesema wanasayansi nchini wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kutafuta suluhu ya
matatizo mbalimbali katika jamii lakini kazi zao zinatambuliwa zaidi nje ya
nchi kuliko zinavyotambuliwa nchini jambo ambalo linaweza kuwavunja moyo.
“Kongamano hilo ni la kujadili na kutafuta suluhu ya matatizo tuliyonayo,
tutumie tafiti za wanasayansi wa ndani badala ya kuwavunja moyo na kila
anayejaribu kwa kutafiti apewe fursa ili aendelee kutafiti zaidi na matokeo
tutayaona,” amesema DKt. Biteko.
Ameongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa wanasayansi na kuwawezesha
watafiti na wabunifu na kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH
imetoa kiasi cha bilioni 32 kwa ajili ya kuimarisha miradi ya utafiti na
ubunifu.
Tangu mwaka 2015 Serikali imeshapokea kiasi cha shilingi bilioni 222.8 kwa
ajili ya kujenga uwezo kwa wanasayansi wabunifu kuendeleza miradi mbalimbali
ambazo zimesaidia kuwajengea uwezo wanasayansi wakiwemo wanasayansi vijana.
Post a Comment