DKT. GWAJIMA AIPA POLE FAMILIA YA GRAISON KENYENYE ALIYEUAWA DODOMA


......................
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima ametoa pole kwa wazazi wa mtoto Graison Kenyenye aliyeuawa na watu wasiojulikana, huku akiwataka wazazi au walezi kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto.

Tukio hilo lilitokea Ilazo Extension jijini Dodoma Desemba 25, 2024, wakati mfanyabiashara Zainab Shaban maarufu Jojo alipomuacha mtoto huyo nyumbani kwa rafiki yake wa kiume ambaye ni Ofisa Uvuvi Mtera, Hamis Mpeta.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi, tukio hilo lilitokea Desemba 25,2024 saa 1.00 asubuhi ambapo Mpeta akiwa na mama wa mtoto Zainab walibaini mtoto huyo kuuawa baada ya kurejea kutoka matembezini.

“Walimkuta mtoto huyo akiwa ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na shingoni amekatwa na kitu chenje nja kali. Katika tukio hilo ni kwamba mama wa mtoto alimwacha chini ya uangalizi dereva bodaboda anayejulikana kwa jina la Kelvin Gilbert,” alisema.

Katika taarifa yake kwenye vyombo vya habari leo Ijumaa Desemba 27, 2024, Dk Gwajima amesema wizara yake imepokea kwa taarifa hizo za masikitiko kwa simanzi kubwa kutokana na mtoto huyo kukatishwa uhai wakati ndiyo kwanza alikuwa anaanza safari ya ndoto za maisha yake.

Source:Mwananchi

0/Post a Comment/Comments