Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba amesema amesikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa Watumishi
watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na gari lao (STL 9923) walipokuwa
wakitekeleza majukumu yao ya kisheria ya kudhibiti magendo na magari
yaliyoingizwa nchini kinyume cha sheria, usiku wa December 5, 2024, katika eneo
la Tegeta kwa Ndevu, Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Waziri Mwigulu leo December
06,2024 imesema “Watumishi hao walikuwa wakifuatilia gari namba T229 DHZ (BMW
X6) lililoingizwa nchini bila kulipa kodi stahiki, natoa kwa wote waliojeruhiwa
na kuwaombea wapate nafuu haraka”
“Wizara ya Fedha inalaani vikali tukio hili na
kuahidi kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika wa uhalifu huu, aidha
TRA itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa mujibu wa sheria”
DKT MWIGULU ALAANI SHAMBULIZI WATUMISHI TRA
.....................
Post a Comment