Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), (wa pili kulia), Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (wa kwanza kulia) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia (Saudi Fund for Development-SFD), Bw. Sultan Al-Marshad, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Mfuko huo na Tanzania, mazungumzo hayo yalifanyika Makao Makuu ya Mfuko huo Mjini Riyadh nchini Saudi Arabia, Kando ya Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, lililofanyika nchini humo.
(Pich ana Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini- Riyadh-Saudi Arabia)
....................
Na Benny Mwaipaja. Saudi Arabia
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu
Nchemba (Mb), ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia (Sadi Fund for
Development-SFD), kwa mchango wake katuika maendeleo ya Tanzania kupitia
ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za maji, afya, nishati
na ujenzi wa miundombinu ya barabasra.
Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo
alipo kutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Fund, Bw.
Sultan Al-Mashard, Kando ya Mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji,
lililofanyika Mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.
Dkt. Nchemba aliyeambatana na
Mawaziri wenzake wawili katika kikao hicho, akiwemo Waziri wa Viwanda na
Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na
Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema kuwa ushirikiano wa
Saudi Arabia na Tanzania uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 sasa, umekuwa wa mfano.
Aliitaja baadhi ya miradi iliyoleta
mageuzi makubwa katika jamii ya Tanzania kuwa ni pamoja na ukarabati wa Mradi
wa Maji mkoani Mara (Usd 15m), Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe
(Usd 25m), na ujenzi wa Barabara za Vijijini Awamu ya Pili-Zanzibar (Usd11.4m).
Aliitaja miradi mingine kuwa ni
Ukarabati na Upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar (Usd 15m) na
kushirikiana na wadau wengine kufadhili Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme wa
msongo wa 220kV kuanzia Benako hadi Kyaka (Usd 105.4m).
Katika Mazungumzo hayo, Dkt. Nchemba
aligusia utekelezaji wa miradi mingine mikubwa ya kimkakati inayoendelea nchini
Tanzania ukiwemo mradi wa Reli ya Kisasa SGR, ambao alisema utakapokamilika
utakuwa kichocheo kikubwa cha biashara na Uchumi katika nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu.
Kwa upande wao. Waziri wa Viwanda na
Biashasra, Mhe. Dkt. Selemani jafo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na
Mipango Zanzaibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, walisema kuwa ushiriki wa Mfuko
wa wa Maendeleo wa Saudi Arabia katika ujenzi wa miradi ya kiuchumi na kijamii
nchini Tanzania utachochea maendeleo ya nchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi
Fund, Bw. Bw. Siultan Al-Marshad, alisema kuwa Mfuko huo uko tayari kuendelea
kuisaidia Tanzania kutokana na uhusiano imara uliopo kwa faida ya wananchi wa
nchi hizo mbili.
Alipongeza hatua kubwa
zinazochukuliwa na Serikali katika kutekeleza miradi muhimu kwa maendeleo ya
nchi akiitaja Reli ya Kisasa inayojengwa kwamba itachochea na kukuza biashara
na usafirishaji wa abiria na mizigo katika eneo la mradi.
Katika kikao hicho Tanzania na Saudi Fund walikubaliana kuunda Timu ya wataalam watakaopitia, kuchambua na kuchakata miradi mbalimbali ambayo Mfuko huo utatoa fedha ili kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia.
Post a Comment