HITILAFU GRIDI YA TAIFA YAPELEKEA KUKOSEKANA KWA UMEME USIKU HUU


***

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema hitilafu iliyojitokeza katikati ya Mfumo wa Gridi ya Taifa leo, tarehe 18 Disemba 2024, majira ya saa 06:12 usiku, imepelekea mikoa inayopata umeme kutoka gridi hiyo kukosa huduma ya umeme.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, TANESCO imesema timu ya wataalamu inaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme katika maeneo yote yanayokosa umeme.

Hata hivyo, TANESCO imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.


0/Post a Comment/Comments