******
Msafara wa watu saba wa timu ya
mchezo wa gofu ya Lugalo Dar es Salaam imeondoka nchini kuelekea Nairobi Kenya
kwaajili ya kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki yatakayoanza kutimua vumbi
Disemba saba mwaka huu.
Mkuu wa msafara wa timu ya gofu ya Lugalo Meja Jenerali Ibrahim Michael
amekabidhiwa bendera na wadhamini wa timu hiyo benki ya KCB ili kuanza safari
hiyo kuelekea Kenya
Amesema wachezaji wake wapo tayari na anaamini watarudi na ubingwa wa michuano
hiyo ya Afrika Mashariki
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka benki ya KCB Bi Frida Shirima amesema benki
hiyo itaendelea kuunga mkono sekta ya michezo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Jumla ya timu 10 kutoka nchi za Afrika Mashariki zimekata tiketi ya kushiriki
katika mashindano hayo baada ya kufanya vizuri kwenye nchi zao huku Mashindano
hayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili na yataanza kutimua vumbi Ijumaa na
kumalizika Jumamosi wiki hii
Post a Comment