MABEHEWA 264 YA MIZIGO YAFIKA DAR ES SALAAM

........................
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema  kwamba mabehewa 264 ya mizigo, yatakayotumika katika Reli ya Kisasa SGR yamewasili katika Bandari ya Dar es Salaam jana  tarehe 24 Disemba, 2024 kutokea nchini China.

Taarifa iliyotolewa na TRC imeeleza kuwa Zoezi la ushushaji kutoka kwenye Meli litakapokamilika litafuatia zoezi la majaribio ambalo litajikita katika kutembeza mabehewa hayo kwenye Reli yakiwa tupu na kisha yakiwa yamebeba mizigo. Mabehewa hayo yatakuwa yanatembea kwa kasi ya kilometa 120 kwa saa.

Majaribio hayo yatakamilika mara tu wataalamu wa Shirika la Reli wakishirikiana na wale wa mkandarasi watakaporidhika kuwa utendaji kazi wa mabehewa hayo umekidhi viwango kulingana na Mkataba. Tarehe rasmi ya kuanza operesheni za mabehewa hayo, Shirika litauujulisha Umma




0/Post a Comment/Comments