Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limeendelea kutoa elimu na
mafunzo kwa askari na wamiliki wa makampuni binafsi ya ulinzi lengo likiwa ni
kuwajengea uwezo askari hao juu ya ukamataji salama,vitendo vya ukatili pamoja
na kufahamu dhana ya Polisi Jamii.
Akihitimisha mafunzo hayo leo Mkuu wa Dawati la Jinsia na
watoto Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP Happiness Temu amewataka wamiliki na
askari wa makampuni hayo ya ulinzi kuzingatia sheria walizofundishwa na
zilizopo katika vitabu vya sheria ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi
Mkubwa.
SP Temu ameongeza kuwa makampuni hayo yanayo nafasi pia
katika kutokomeza ukatili mahala pa kazi na jamii kwa ujumla huku akiwaomba
kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutomeza vitendo vya ukatili
Sambamba na hilo amewaomba kuendelea kufichua uhalifu na
wahalifu ili Mkoa wa Arusha uendelee kuwa na sifa nzuri ya kupinga vitendo
vyote vya uhalifu,kitendo ambacho kitachochea na kushawishi wageni wa ndani na
nje ya nchi kutembelea Mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii hapa nchini.
Post a Comment