MANARA AONYWA NA JESHI LA MAGEREZA

****
Jeshi la Magereza limetoa onyo na kuwataka wananchi kuacha kutoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza au kudharau Mamlaka yake.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi Hilo, Elizabeth Mbezi, baada ya kipande cha video kilichosambaa mtandaoni kikimuonesha, aliwahi kuwa Msemaji wa Simba na Yanga Haji Manara akitoa maneno yasiyo ya kiungwana baada ya kuombwa kutoa gari lake mbele lililozuia gari la Jeshi la Magereza.


0/Post a Comment/Comments