Picha ya pamoja Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele pamoja na Taasisi za Serikali zinazofanya katika mpaka wa Sirari ,Mawakala wa Forodha
********
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amewataka
mawakala wa Forodha katika Mpaka Sirari kuzingatia sheria katika kufanya kazi
mpakani hapo.
Meja Gowele ameyasema hayo wakati akizungumza katika
mkutano wa Mawakala wa Forodha uliondaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli
Tanzania TASAC uliofanyika katika Ofisi za TRA Sirari wilayani Tarime mkoani
Mara.
Amesema kuwa Sheria zipo ambazo zinaongoza kazi ya
Uwakala wa forodha hivyo lazima zifuatwe
katika kuendelea nchi kupata mapato kwa
ajili ya maendeleo mbalimbali.
Meja Gowele amesema kuwa mawakala wa Forodha
wanatakiwa kuwa na ofisi ambazo zitasaidia TASAC kuwafikia na wakati
changamoto zinapotokea kufanya urahisi
wa kuzitatua.
Amesema kuwa kutokana na changamoto zinazojitokeza kwa kuwa na mawakala ambao
hawajasajiliwa amewataka kuwa na vitambulisho ambavyo watatumia katika kufanya
kazi katika eneo la mpaka wa Sirari kati ya Tanzania na Kenya.
Hata hivyo amesema katika mpaka huo kuna watu
wanafanya uwakala wa forodha
hawajasajiliwa na kufanya kuharibu taswira kwa watu waliopo kisheria
ambapo mapato yao yanapotea kutokana na kuwa na hao mawakala wasiosajiliwa.
Mtakwimu Mwandamizi wa TASAC Athman Athman amesema
kuwa mawakala wa forodha sheria ziko wazi katika kufanya kazi hiyo na
wasipofuata sheria hatua zinachukuliwa.
Amesema kuwa katika kuhakikisha mawakala wanaotoa
huduma za forodha TASAC kazi yake kutoa elimu katika kuwa na mawasiliano ambayo
yanaboresha kazi zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uwakala wa
Forodha ya Emaus Logistics Tanzania
Limited Maryam Muhambo amesema
changamoto zinatokana katika Mawakala wa Forodha ni elimu na kuiomba TASAC
kufanya kikao na Viongozi Chama Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFF) ambao watakwenda kutoa elimu
kwa wananchama wao.
Maryam amesema kuwa misingi ya kufanya kazi za uwakala
wa forodha hivyo kazi ya mawakala ni kufuata ili kuepusha migongano na Taasisi
za Serikali zinazodhibiti kazi hiyo.
Nae Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji katika Mpaka wa
Sirari Deodatus Sanda amesema kuwa mawakala wataofanya udanganyifu watachukuliwa
hatua.
Amesema ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Kenya
uendelee kwa watu kutembea kilomita 10 kwa kila nchi na nje hapo hatua
zitachukuliwa.
Amesema kwa madereva wanaoingia na magari biashara
wanatakiwa kulipa na sio kutumia ujirani mwema wa kutembea kwa miguu.
Kaimu Meneja wa Forodha wa TRA Abdallah Salum amesema
kuwa kazi wanaendelea kushirikiana na mawakala wa Forodha kufuata taratibu za
kulinda mawakala wa Forodha kwa
kutoruhusu watu wengine wasiokuwa na utalaam kufanya kazi hiyo.
Picha ya pamoja Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele pamoja na Taasisi za Serikali zinazofanya katika mpaka wa Sirari ,Mawakala wa Forodha.
Mtakwimu Mwandamizi wa TASAC ,Athuman Athuman akizungumza kuhusiana na matakwa ya Sheria ya Uwakala wa Forodha kwa mawakala wa Forodha Sirari mpaka wa Tanzania na Kenya.
Post a Comment