MKURUGENZI OFISI YA HAZINA AFARIKI DUNIA AJALINI NA BINTIYE

****
 Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Amos Lengael Nnko amefariki dunia kwa ajali ya gari. 

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu kupitia taarifa yake, amesema Nnko aliyekuwa akisafiri na familia yake amefikwa na umauti 

Same mkoani Kilimanjaro jana Jumapili, Desemba 22,2024.

Kwa mujibu wa Mchechu ajali hiyo pia imechukua uhai wa binti yake Maureen huku mkewe Agness na watoto Marilyn, Melvin na wanafamilia wengine Sylvana wakijeruhiwa. 

Mchechu alisema wanafamilia hao kwa sasa wanapatiwa matibabu katika Hospitali za KCMC na Mawezi mjini Moshi.


0/Post a Comment/Comments