Mtoto anusuriwa baada ya kukaa
baharini kwa siku tatu katika kisiwa cha Lampedusa cha Italia.
Mtoto wa kike wa miaka 11
kutoka Sierreleone, aliyenusurika peke yake katika ajali ya boti aliokolewa
usiku wa kuamkia Jumatano baada ya kukaa kwa siku tatu baharini katika
kisiwa cha Italia cha Lampedusa.
Shirika la hisani la uokozi la
Kijerumani limesema wafanyakazi wake wa melini waliokuwa njiani kuelekea kwenye
tukio jingine la dharura, walisikia sauti baharini ya mtoto huyo majira ya saa
tisa alfariji.
Aliokolewa akiwa amevalia jaketi
maalum la kumsadia kutozama huku akiwa anaelea baharini akiwa juu ya boya la
kuogelea.
Mtoto huyo aliwaeleza shirika la
uokoaji la kijerumani kwamba alisafiri kutoka mji wa Sfax Tunisia kwa
boti ya kuundaunda akiwa na watu wengine 45 na ilizama kutokana na dhuruba ya
baharini.
Chanzo:Dwkiswahili
Post a Comment