MUGANA HOSPITAL POKEENI MAUA YENU HUDUMA BORA NA USAFI WA MAZINGIRA


****

Leo MDAU nimepata nafasi ya kutembelea Hospitali ya Mugana iliyoko Mkoani Kagera inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba hakika nimefurahishwa sana na watoa huduma, wana kauli nzuri, huduma nzuri lakini zaidi ya yote wanatunza mazingira kwa kiwango kikubwa.

Naiomba TAMISEMI ipite hapo itoe maua yake aidha naliomba Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) watembeleeni muwatie moyo kwani kazi yao ni njema sana katika utoaji huduma na usimamizi wa mazingira ya ndani na nje. 

Korido zote ni safi, majani na maua vimetengenezwa vizuri, upandaji wa miti unavutia sana,  ukienda wodini private na general utapenda mwenyewe...usafi. Hapa Matron  Sister Liberata Damian Canossian chukua maua yako.

Nimpongeze pia Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Mgana Dkt. Emanuel  Simeo alafu ni kijana

na Menejimenti yake pamoja watumishi wote kwa kazi nzuri. 

Mdau nawatakia *HERI YA MWAKA MPYA*



0/Post a Comment/Comments