NABII wa Madhabau ya hatma,Clear Malisa,amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,kwa serikali yake kutoa uhuru wa kuabudu bila kuchagua dhehebu wala Dini.
Kiongozi huyo wa kiroho ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuzungumzia mkesha mkubwa unaotarajia kufanyika leo kanisani hapo Ubungo Jijini hapa.
"Rais Samia amekuwa na ushirikiano mkubwa kwetu viongozi wa dini,tunamshukuru kutobagua dhehebu lolote"Amesema Malisa.
Hata hivyo,Malisa ameutabiri mwaka 2025 utakuwa mwaka wa neema zaidi kwa Taifa la Tanzania katika nyanja ya uchumi ikiwemo kupanda kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola za Kimarekani.
Akizungumzia suala la Utabiri anaofanya,kiongozi huyo kwa kiroho amesema ni Utashi ambao Mungu amempa na kuhaidi kutoa utabiri juu ya mambo mbalimbali kuhusu uchaguzi mkuu wa hapo mwakani kupitia kwenye mkesha utakaofanyika kanisani hapo.
Sanjari na hayo,Malisa ametumia mkutano huo kuwataka watanzania kipindi hiki cha mkesha huu wa mwisho wa mwaka kujitokeza kwenye nyumba za Ibada kufanya maombi na kumshukuru Mungu.
Post a Comment