Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo (Mb.) ameeleza kuwa Serikali imejipanga kuzisimamia na kuziwezesha Halmashauri hususan za mipakani kuwa kiungo muhimu kwenye masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za Mtangamano.
Mhe. Londo ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi
mkoani Tanga yakutembelea Kituo cha Utoaji Huduma kwa Pamoja Mipakani cha Horohoro/Lungalunga (Horohoro One Stop
Boarder Post- OSBP)
Ziara hiyo ililenga kuangalia utekelezaji wa shughuli za
Himaya Moja ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na hali ya
miundombinu na uendeshaji wa OSBP hiyo.
Katika ziara hiyo,
Mhe. Londo amepata fursa ya kuzungumza na Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali
zinazotoahuduma katika OSBP na kutoa wito kufanya kwa uadilifu na weledi
ili kutimiza azma ya Serikali ya
kuhamasisha mtangamano kwa lengo la kukuza muingiliano na bishara za mipakani.
Mhe. Londo ameahidi
Serikali itaendelea kutatua changamoto za kiuendeshaji zinazozikabili OSBP hiyo pamoja na changamoto wanazokutana
nazo wafanyabiashara katika mpaka huo na mingine nchini.
"Jumuiya ina fursa nyingi ambazo hazijatumika ipasavyo
kwa manufaa ya wafanyabiashara wetu ni vema halmashauri zikabuni mbinu na
mikakati ya makusudi kuwawezesha Wafanyabiashara hususan wadogo kuongeza
thamani ya bidhaa zao ili ziweze kuuzwa bila vikwazo katika nchi za
Jumuiya", alisema Mhe. Londo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Londo alipata fursa ya kukutana na
viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga akiwemo Mkuu wa Mkoa, Mhe. Balozi Batilda
Buriani, Afisa Tawala wa Mkoa, Bi. Pili Mnyema, wawakilishi kutoka Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Wawakilishi
kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga pamoja na
Wafanyabiashara na Mawakala wa Forodha wanaofanya shughuli zao katika mpaka wa
Horohoro.
Post a Comment