HATIMAYE NONDO APATIKANA AMETUPWA OFISI ZA ACT

..............,..

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Abdul Nondo amepatikana usiku huu wa leo Jumapili, Desemba 1, 2024.

Nondo alichukuliwa na watu wasiojulikana alifajiri ya leo stendi ya mabasi Magufuli aliposhuka kwenye basi akitokea mkoani Kigoma, na amekutwa akiwa ametupwa pembeni mwa makao makuu ya chama hicho yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mwananchi limezungumza na Ado ambaye amesema kwa kifupi ni kweli amepatikana.

Taarifa zimedai Nondo ametupwa na watu wasiojulikana ofisini na hali yake si nzuri.
 

0/Post a Comment/Comments