PROF. MLAMA AWAASA WAANDISHI WA TAMTHILIYA KUWASILISHA MISWADA KWA TUZO ZA MWALIMU NYERERE


*****

Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama, ametoa rai kwa waandishi wa Tamthiliya nchini kuwasilisha miswada yao kwa ajili ya kushindinishwa kwenye tuzo ya mwaka 2024/2025.

Wito huo ameuotoa leo tarehe 10/12/2024 jijiji Dar es salaam katika kikao maalumu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Dkt. Gervas Kasiga, Mkurugenzi Mku wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET), Dkt. Aneth Komba, pamoja na wajumbe wa menejimenti ya TET na baadhi ya waandishi wa tamthiliya nchini.

Prof. Mlama amewaomba waandishi hao kuwasilisha miswaada yao kwa wingi ili kuhakikisha tamthiliya zenye maadili ya kitanzania zinaendelea kukua kwa wingi na kuchangia kukuza lugha ya Kiswahili.

“Nawaomba sana hii ni fursa kubwa sana kwenu wataalamu wa tamhiliya nchini, hamasishaneni wataalamu wengine wa tamthiliya ili wote muweze kuleta miswada tupate maadiko mengi “amesema Prof. Mlama.

Aidha, Prof. Mlama amesema tayari wameanza kupokea miswada ya tamthiliya lakini akaomba iweze kuwasilishwa zaidi na kuingia katika zoezi la kushindanishwa huku pia akiwaisisitiza waandishi wa Riwaya, Hadithi za Watoto na Ushairi nao kuendelea kuwasilisha kazi zao ambapo mwisho wa kuwasilisha ni tarehe 30/12/2024.

Kwa upande wake ,Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kasiga, ameeleza kuwa imekuwa jambo jema kwake na waandishi wa filamu kujumuika kwa pamoja na kamati ya Tuzo na TET kuweza kuzungumzia suala hilo ili kuhamasisha wahusika kuweza kuwasilisha mawasilisho yao na kupata maandiko mazuri yatakayioshiundishwa.

“Imekuwa vyema sana kwetu kupata nafasi hii, tutaitumia vyema kuhamaisha wahusika wote wa tamthilya nchini kuweza kuleta maandiko yao ambayo yataweza pia kukuza maadili na lugha ya Kiswahuli “amesema Dkt. Kasiga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba, amewaomba waandishi bunifu kuwasilisha kazi zao kabla ya tarehe iliyopangwa.

Tuzo za mwaka 2024/2025 inahusisha njanja nne ambazo ni Hadtihi za Watoto, Ushairi, Riwaya na Tamthiliya.









0/Post a Comment/Comments