Dar es Salaam.
Amesema, mwaka 2022 Februari 10, TEA ilisaini makubaliano maalum ya ushirikiano na Shirika la BRAC - Maendeleo Tanzania ambalo ni mdau muhimu wa maendeleo katika Sekta ya Elimu hapa nchini na kupitia ushirikiano huo, jumla ya Kompyuta 60 na Vishkwambi 60 vyote vyenye thamani ya Tsh, 132.6 zilitolewa kwenye shule tatu za Sekondari za Wilayani Temeke.
Aidha, ameipongeza BRAC Maendeleo Tanzania kwa kufadhili na kugharamia programu hiyo ya kuendeleza ujuzi yaani ‘‘Skills for their Future’’ iliyolenga kuwajengea walimu pamoja na wanafunzi uwezo wa kutumia TEHAMA katika Shughuli zao mbalimbali ikiwemo shughuli za kitaaluma pamoja na bunifu kwa kuwanufaisha wanafunzi 1,922 na walimu 64
Akiongea kwa niaba ya shule nufaika Mkuu wa Shule ya Wailes Mwl. Daudi Kassenga amesema, mradi huo wa TEHAMA umekuwa na manufaa makubwa kwa walimu pamoja na wanafunzi kitaaluma kwani umewasaidia kubuni njia mbalimbali za kufundisha na kuandaa masomo kiurahisi.
‘‘Kabla ya huu mradi, shule zetu za sekondari zilikuwa hazina Kompyuta wala makataba, lakini kupitia mradi huu, kila shule imepata Kompyuta 20, vishkwambi 20 na kukarabatiwa chumba kimoja cha kuhifadhia vifaa hivyo vya TEHAMA. Amesema Mwl. Kassenga’’
Nae Anuary Josephati mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Miburani amesema, amefaidika sana na mradi huo kwani wakati programu ya mafunzo inaanza alikuwa kidato cha kwanza na ndo ilikuwa mara yake ya kwanza kujifunza Kompyuta.
‘‘Mimi nilikuwa
kidato cha kwanza wakati mafunzo yanaanza hivyo nilijiwekea nadhiri kwamba
lazima nisome na hadi sasa nimejifunza kubuni na kutengeneza mifumo mbalimbali
inayoweza kutumika kurahisha kazi kwenye jamii lakini pia nimejifunza
ujasiriamali kupitia TEHAMA. amesema Anuary’'
Sambamba na hayo amesema, pia kumekuwepo na vikwazo vya kijamii na kitamaduni ambapo wazazi wanapendelea wavulana zaidi kulinganisha na wasichana hasa katika elimu, na hiyo imesababisha idadi ndogo ya wasichana kupata mafunzo ya kidigitali, na kupata ujuzi unaohitajika wa kufanya kazi za teknolojia.
Amesema kutokana na
changamoto hizo, ndiyo maana wakaamua kuanza kutoa mafunzo hayo ya TEHAMA
mashuleni ili wanafunzi wa kike wapate nafasi ya kunufaika na programu
mbalimbali zitakazotolewa kipindi cha mafunzo.
"Wasichana
wetu sasa wanao uwezo wa kutumia teknolojia kujiendeleza kimasomo na kuboresha
maisha yao ya kila siku". Ameeleza
1. Mwakililishi wa Mkurugenzi wa BRAC Maendeleo Tanzania Bi. Kalunde Simba akitoa taarifa ya utekelezaji mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future katika hafla fupi ya kufunga na kukabidhi mradi huo katika shule tatu za Sekondari Wilayani Temeke.
1. Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bi. Niconia Amosi akitoa salamu za Mkurugenzi katika hafla ya kufunga na kukabidhi mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future katika shule tatu za Sekondari Wilayani Temeke.
1. Baadhi ya wanafunzi walionufaka na mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future kutoka shule za sekondari za Karinuni, Miburani na Wailes wakiwa katika hafla ya kufunga na kukabidhi mradi huo iliyofanyika Wailes Shuleni.
1. Baadhi ya wanafunzi walionufaka na
mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future kutoka shule za
sekondari za Karinuni, Miburani na Wailes wakiwa kwenye picha ya pamoja na
wafadhili wa mradi.
Post a Comment