RAIS WA ZANZIBAR DK. MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA SALA YA MAITI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika kubeba jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Bi. Mtumwa Ali Salum, Mama Mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Ame Chum, kwa ajili ya Ibada ya Sala ya Maiti iliyofanyika katika Masjid Mamiali Saateni Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-12-2024.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Maiti ya Marehemu Bi.Mtumwa Ali Salum. Mama Mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Othman Ame Chum(kushoto kwa Rais) ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh  Omar Kabi, iliyofanyika katika Masjid Mamiali Saateni Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-12-2024 na kuzikwa Kijijini kwao Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuka na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Bi. Mtumwa Ali Salum, Mama Mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Ame Chum,(kushoto kwa Rais) ikisomwa na Sheikh.Dr. Muhyddin Ahmad Khamis (Maalim Siasa) baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti iliyofanyika katika Masjid Mamiali Saateni Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-12-2024.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Bi. Mtumwa Ali Salum, Mama Mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Ame Chum, maziko yaliyofanyika Kijijini kwao Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati Unguja leo 9-12-2024.(Picha na Ikulu)

0/Post a Comment/Comments