SERIKALI KUENDELEA KUJENGA UCHUMI WA KIDIJITALI -RAIS SAMIA


 *****

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan amesema mwaka 2024 serikali imeendelea na jitihada za kujenga uchumi wa kidigitali kupitia matumizi ya Tehama ambapo kupitia kufanikisha Hilo wameunda Wizara mahususi ya Tehama na wamezindua mkakati wa uchumi wa kidigitali.

Rais Samia amesema hayo Leo Zanzibar wakati akizungumza na wananchi akitoa salamu za mwaka mpya 2025.

Rais Samia amesema kuwa Miongoni mwa mipango ya baadae katika kutekeleza mkakati huo ni kuhakikisha Kila Mtanzania anatambulika kwa kutumia jamii Namba,itakayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

0/Post a Comment/Comments