Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeipongeza Kampuni ya ukandarasi kutoka nchini
China ya CRJE (East Africa) Ltd kwa ufanyaji kazi uliotukuka huku ikiahidi
kuendelea kukuza mahusiano yaliyodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na China
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas
Ndumbaro wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Uwajibikaji kwa Jamii ya CRJE kwa
ushirikiano na Hoteli ya Johari Rotana.
Hafla hiyo ilihudhuliwa na wageni mbalimbali akiwemo, John
Mnali, Mkurugenzi wa Ukuzaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku na balozi wa China
nchini Tanzania Chen Mingjian.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Ndumbaro, ofisa mwandamizi
katika wizara hiyo Shoma Philip Ndono, alisema Kampuni ya CRJE imeongeza kwa
kiasi kikubwa uhusiano mwema wa urafiki kati ya China na Tanzania.
"Tunashukuru na tunatamani urafiki wetu uendelee kudumu kwa muda mrefu
ujao.”Alisema kampuni hiyo ya ukandarasi kutoka China ipo Tanzania kwa zaidi ya
miaka 55 na imefanya kazi nzuri kwa ustawi wa jamii ya Watanzania."CRJE
wamehafanya miradi zaidi ya 200 na wametoa mchango mkubwa katika kutoa ajira
kwa watanzania pamoja na utekelezaji wa uwajibikaji kwa jamii" alisema.
Akizungumza kando ya hafla hiyo, Mkurugenzi wa Uhamasishaji
Uwekezaji wa TIC John Mnali aliishukuru kampuni hiyo ya China kwa kuzindua
ripoti hiyo na kuitaka kuvuka mipaka na kusaidia changamoto zinazoikabili
jamii.Alisema kampuni hiyo imekuwa ikisaidia jamii katika elimu, miundombinu na
utunzaji wa mazingira jambo ambalo lina mchango mkubwa katika malengo ya
maendeleo endelevu ya Tanzania.Mnali alisema uwazi na uwajibikaji ni msingi wa
kampuni hiyo ya kutoka China akiyataka Makampuni mengine kuiga mfano
ulioonyeshwa na CRJE.Aliitaka kampuni hiyo kuendelea kufanya kazi kwa karibu na
serikali na taasisi nyingine kwa manufaa ya nchi ya Tanzania a China.Aliongezea
kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuhakikisha kuwa wawekezaji wanafanya
shughuli zao chini ya mazingira mazuri.
Katika hotuba yake, Balozi wa China nchini Tanzania, Chen
Mingjian alisema: “Kwa niaba ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, napenda kutoa
pongezi na shukrani zetu za dhati kwa CRJE kwa mchango wao katika uwajibikaji
wa kijamii.Balozi huyo aliendelea kusema: “CRJE imefanya mengi makubwa nchini
Tanzania kwa miaka 55. Ilianzishwa mwaka 1969, ilihusika katika ujenzi wa reli
kubwa ya Tazara, mradi mkubwa zaidi kwa
ruzuku kutoka China.”Alibainisha miradi mingine mikubwa ambayo imefanywa na
CRJE ni pamoja na ujenzi wa daraja la Nyerere, ukumbi mpya wa mijadala wa
Bunge, kituo cha mikutano cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Dodoma, Nyerere Foundation
Square na Shule ya Uongozi ya Nyerere. “Wameshajenga zaidi ya mita za mraba
milioni 3, miradi mikubwa 200 nchini Tanzania.”
Aliongezea: "CRJE imeshatunukiwa tuzo ya mkandarasi
bora wa kigeni mara tatu nchini Tanzania, na tuzo ya Luban mara tatu - Tuzo ya
Oscar ya China kwa ubora katika ujenzi." Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
CRJE Jiang Yuntao alisema kuwa kuinduliwa kwa Ripoti yao ya Uwajibikaji kwa
Jamii (CSR) ni hatua muhimu ya kweli katika maendeleo ya kampuni yao na ni
kielelezo cha dhamira ya kufanya kazi bega kwa bega na jamii ya
watanzania.Yuntao alisisitiza: "Kwa miaka mingi, tumejitolea sio tu kwa
ujenzi wa miundombinu lakini pia uwekezaji, uwekezaji wa jumla ya zaidi ya dola
milioni 260.”Alimalizia: “Ripoti yetu hii ya CSR haiakisi tu kazi tuliyofanya
huko nyuma bali pia ni ahadi ya kuendelea kuchangia ukuaji na maendelea kwa
nchi ya Tanzania. Tumejitolea kufanya kazi kwa karibu na serikali ya Tanzania,
sekta binafsi, na jumuiya za mitaa ili kusaidia maendeleo ya taifa na kuboresha
ubora wa maisha kwa watanzania.
Mwisho
Post a Comment