.......................
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi akemea vikali uharibifu wa viti uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba Sports Club ya Tanzania na CS Sfaxien ya Tunisia, Desemba 15, 2024.
Prof. Kabudi amemuagiza katibu wa Wizara hiyo kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia klabu ya Simba na kuwanakili Shirikisho la mpira nchini (TFF) kwa makusudi ya kuwataka walipie gharama za uharibifu zilizofanywa katika mchezo huo wa kombe la shirikisho Afrika.
Pia Prof. Kabudi ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka wote waliohusika kwenye uharibifu huo wachukuliwe hatua za kisheria.
Post a Comment