Tanzania ina jumla ya marubani 603, míongoni mwao
ikiwa ni wazawa 344, wageni 259 huku ikiwa na uhitaji wa jumla ya marubani 755
na upungufu wa marubani 152.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA), Bw. Salim Msangi wakati akiongoza zoezi la kuwapongeza vijana wa
kitanzania waliobahatika kupata udhamini wa kusomea urubani na Uhandisi wa
Ndege. Desemba 7, 2024 jijini Dar es Salaam.
Alisema kabla ya hapo, awali wakati mfuko umeanza walisomeshwa marubani wanne,
ambao kwasasa wameajiriwa na mashirika mbalimbali, hivyo kwa ujumla mfuko hadi
sasa umesomesha wanufaika 23.
Bw. Msangi alieleza katika kuadhimisha wiki ya usafiri wa anga duniani, Mamlaka
kupitia kitengo cha uhusiano na mawasiliano pamoja na watalaam wake kutoka
Idara mbalimbali
ilitumia wiki hiyo kujenga uelewa juu ya kazi za Mamlaka katika kuelekea miaka
80 ya usafiri wa anga duniani, hii ikienda sambamba na kutoa uelewa kwa jamii
juu ya matumizi ya ndege nyuki (drones) ikiwa ni sheria na taratibu za vibali
na leseni kumiliki ndege nyuki hizo.
Alisema elimu hiyo ilitolewa katika vyombo vya habari
Radio na televisheni ikiwemo Clouds FM, Radio One FM na Kituo cha
Azam TV.
Alisema mbali na vyombo vya habari pia walitembelea baadhi ya shule za
sekondari zilizopo mkoa wa Dar es
Salaam ikiwa na lengo la kuelimisha na kuhamasisha wanafunzi waliopo mashuleni
kusoma kwa bidii na kuweza kuingia kwenye sekta ya anga nchini ambayo
inakabiliwa na uhaba wa wataalam wazawa.
Shule zilizotembelewa ni
Shule ya Sekondari Kibasila iliyopo wilaya Temeke, Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Jangwani iliyopo wilaya ya llala, Shule ya Sekondari Makongo
iliyopo wilaya ya Kinondoni na Shule ya Sekondari Kwemba iliyopo wilaya ya
Ubungo
Pia alisema wiki hiyo ilimalizwa semina kwa njia ya mtandao (Webinar) ikiwa na
ujumbe ‘meet the professionals of aviation’ iliyozungimzia maendeleo mbalimbali
yaliyofikiwa katika sekta usafiri wa anga nchini Tanzania. Ambapo hoja
mbalimbali ziliibuliwa na kufanyiwa majadiliano.
Post a Comment