Tanzania kuzindua Tuzo za Utalii na Uhifadhi Disemba 20, 2024 mwaka huu kuenzi umahiri
katika maeneo hayo.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi
ameyasema hayo leo Jumapili Disemba 8, 2024, jijini Dar es Salaam alipokutana
na waandishi wa habari na kueleza kuwa tuzo hizo zitazinduliwa jijini Arusha na
zitapabwa na Burudani mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
“Mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa katika sekta ya
utalii, hivyo Disemba 20 hatutazindua tuzo tu bali itakuwa siku yakusherehekea
mafanikio katika sekta hii ikiwemo kushinda Tuzo ya World Travel Awards kama
Kivutio Bora Zaidi Duniani Kwa Utalii wa Safari 2024,” alisema Dkt. Abbasi.
Amesema tuzo hizi zinalenga kuwaheshimisha wadau makampuni na pia wahifadhi ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii na kuendeleza uhifadhi nchini.
Post a Comment