Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imetumia Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga
Duniani(ICAD) kushiriki katika mbio za Marathon zilizoandaliwa na Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM).
Mbio hizo zilizoongozwa
na Mhe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko,
zilihudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Jakaya Kikwete .
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani
(ICAD) ambayo kilele chake ni Desemba 7,2024. Maadhimisho ya mwaka huu pia
inatimia miaka 80 tangu siku hii ilipoanza kuadhimishwa mnamo Desemba 7 mwaka
1944.
Watumishi wa TCAA licha ya kufanya kazi zao za ki udhibiti na kuongoza ndege pia hushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni hatua ya kuweka afya katika hali bora wakati wote.
Post a Comment