******
Timu ya Gofu ya wachezaji wanne ya The Tanzanite imeondoka kuelekea nchini Kenya kwenye kilele cha mashindano ya KCB East Africa Golf Tour 2024 yatakayo zikutanisha timu kutoka mataifa matano ya Afrika Mashariki, ambayo ni wenyeji Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda pamoja na Burundi.
Mashindano hayo yatakuwa na zawadi nono kama KShs milioni 1 kwa mshindi wa jumla na nyumba yenye thamani ya KShs milioni 2.1 kwa atakayepiga Hole-in-One!The Tanzanite Team ni muunganiko wa washindi wanne wa michuano KCB East Africa Golf Tour kwa Tanzania iliyofanyika katika klabu ya Gofu ya Lugalo mwezi Agosti mwaka huu na inaundwa na washindi ambao ni Meja Jenerali Ibrahim Mhona, Peter Mlewi, Hadija Suleiman, pamoja na Hawa wanyeche.
KCB Bank inajivunia kuwa mdau mkubwa wa michezo kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha mshikamano, kuendeleza afya, na kuleta fursa kwa jamii.
Kwa miaka mingi, Kcb imeendelea kusaidia shughuli mbalimbali za michezo ikiwa ni nyenzo muhimu ya kuchochea maendeleo na kuimarisha mshikamano.
Post a Comment