UWEPO WA KIMBUNGA “CHIDO”KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR

.....................

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga “CHIDO” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

‎Kwa mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Mamlaka hiyo imeeleza kuwa  mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kinatarajiwa kuelekea maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji katika kipindi cha siku nnezijazo(tarehe 13 hadi 16 ya mwezi Disemba, 2024).


0/Post a Comment/Comments