WADAU WASISITIZWA KUENDELEA KUPAZA SAUTI UTUNZAJI RASILIMALI ZA MAJI

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala akikabidi Tuzo na cheti kwa wadau walioonyesha mchango wao katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi raslilimali za maji,katika hafla ambayo imeandaliwa na Shirika la Shahidi wa Maji na kufanyika Mkoani Morogoro.

Mkurugenzi wa Shirikala Shahidi wa Maji Abel Dugange akizungumza katika hafla utoaji Tuzo na Vyeti kwa wadau walioonyesha mchango wao katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi Raslilimali za Maji ambayo imeandaliwa na Shirika la Shahidi wa Maji na kufanyika Mkoani Morogoro.

Meneja wa Program Shahidi wa Maji Pendo Hyera akizungumza katika hafla ya katika hafla ya utoaji Tuzo na Vyeti kwa wadau walioonyesha mchango wao katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi Raslilimali za Maji ambayo imeandaliwa na Shirika la Shahidi wa Maji na kufanyika Mkoani Morogoro.

Afisa wa Program Shahidi wa Maji John Muma akieleza jambo katika hafla ya utoaji Tuzo na Vyeti kwa wadau walioonyesha mchango wao katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi Raslilimali za Maji ambayo imeandaliwa na Shirika la Shahidi wa Maji na kufanyika Mkoani Morogoro.

Mhandisi Bodi ya Maji Bonde la WamiRuvu Joseph Kwiitiga akizungumza katika hafla ya utoaji Tuzo na Vyeti kwa wadau walioonyesha mchango wao katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi Raslilimali za Maji ambayo imeandaliwa na Shirika la Shahidi wa Maji na kufanyika Mkoani Morogoro.

Baadhi ya wadau mashahidi wa maji ambao wameshiriki katika hafla ya utoaji Tuzo na Vyeti kwa wadau walioonyesha mchango wao katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi Raslilimali za Maji ambayo imeandaliwa na Shirika la Shahidi wa Maji na kufanyika Mkoani Morogoro.

........,........

 

NA MUSSA KHALID

 

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Shahidi wa Maji katika mapambano ya uelimishaji jamii kuhusu utunzaji na  uhifadhi wa Rasilimali Maji.

 

Hayo yamebainishwa Mkoani Morogoro katika hafla maalum ya utoaji wa tuzo na Cheti kwa wadau walioonyesha mchango wao katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi raslilimali za maji.

 

Akizungumza Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amelipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani maji ndio mzunguko wa uhai wa binadamu.

 

‘Tunafahamu maji ni uhai,ni usalama bila ya maji hakuna jambo lolote,kwani hata umeme na viwanda unategemea maji,hivyo lazima tutunze vyanzo vyetu vya maji kwa wivu mkubwa sana na tuvizungumze kwa upana watu watuelewe na sio jukumula serikali pekee bali kwa jamii nzima inayotuzunguka’amesema DC Kilakala

 

Amesisitiza kuendelea kukemewa na kuelimisha watu wenye nia ovyo ya kujinufaisha wao kwani wanavyoahiribu vyanzo vya maji wanawakosea wanaoutumainia mto huo.

 

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Shirikala Shahidi wa Maji Abel Dugange amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu ya mapambano dhidi ya uharibifu wa rasilimali maji ambapo zaidi ya watanzania Milioni Mbili na Laki Tano wamefikiwa na mradi huo.

 

‎Amesema kuwa kama Taasisi wanatambua kwamba Maji ni Kila kitu katika maisha ya binadamu kwani bila.maji hakuna maenendeleo  ya kiuchumi,na bila Maji haiwezekani kuzungumzumzia usawa wa kijinsia.

 

Mkurugenz huyo ameeleza kuwa Malengo yao katika miaka ijayo ni kuwafikia wananchi zaidi ya laki Tano watakaokuwa na uwezo wa kuhamasisha namna ya utunzaji wa rasilimali Maji katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Akisoma taarifa ya Shahidi wa maji Mbele ya Mgeni Rasmi,Meneja wa Program Shahidi wa Maji Pendo Hyera amesema program hiyo ijulikanayo kama Sauti za Maji ilianza mwaka Mwaka 2023 ambapo Shirika limewajengea uwezo mashahidi wa maji kushiriki kikamilifu katika kupaza sauti za uharibifu wa rasilimali maji.

 

Amesema kupitia mradi huo Wameweza kupaza Sauti kupitia vyombo vya habari na mikutano kuhusu utunzaji rasilimali za Maji na kufanya utatuzi mbalimbali lakini pia wameweza kuongeza vijana na wanawake kushiriki katika mapambano hayo.

 

Naye Mhandisi Bodi ya Maji Bonde la WamiRuvu Joseph Kwiitiga amesema wanaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakisha kuwa vyanzo vya maji zinaendelea kulindwa.

 

Ameipongeza Shahidi wa Maji kwa kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kushiriki namna ya kulinda na kuvitunza vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali.

 

‎Katika Hafla hiyo Shirika la Shahidi wa Maji limetoa vyeti na Tuzo kwa makundi mbalimbali,yakiwemo ya wadau kutoka Morogoro pamoja na Dar es salaam sambamba na waaandishi wa habari ambao wamekuwa wakionyesha mchango mkubwa katika mapambano ya uharibifu wa rasilimali za maji.

0/Post a Comment/Comments