BAKHRESA ASHINDA TUZO MLIPA KODI MWENYE HADHI YA JUU


Mmiliki wa kampuni za Bakhresa Group, Said Salim Bakhresa ametunukiwa tuzo ya hadhi ya juu ya mlipa kodi wa hiyari nchini Tanzania katika hafla ya siku ya utoaji tuzo kwa walipakodi bora kwa mwaka 2023/24.

Tuzo hiyo ambayo amekabidhiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na kufanyika Masaki, Dar es Salaam, imemtambua Mzee Bakhresa kuwa mlipaji wa hiyari wa kodi aliyechangia kiwango kikubwa zaidi cha kodi serikalini mwaka 2023/2024.

Bakhresa Group inamiliki kampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na viwanda vya uzalishaji wa chakula, vinywaji baridi, usafirishaji baharini, vyombo vya habari, utalii na huduma za kifedha.






 

0/Post a Comment/Comments