******
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amemuaga Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yasushi
Misawa anayetarajia kumaliza muda wake wa uwakilishi Januari 17, 2025.
Kwa upande wake Balozi Misawa ameishukuru Wizara kwa kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake ya kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Japan kwa kipindi alichohudumu cha takribani miaka miwili na miezi saba hapa nchini.
Halikadhalika, Mhe. Waziri Kombo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kudumisha kazi nzuri aliyoifanya na itampatia ushirikiano wa kutosha Balozi mpya wa Japan atakayepangwa kuhudumu Tanzania.
Post a Comment