Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema bajaji na bodaboda hazitaruhusiwa kuingia katikati ya jiji katika kipindi cha Mkutano wa Nishati Afrika utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo, Jumamosi Januari 25, 2025, na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema kutokana na ugeni huo, barabara hizo zitafungwa kuanzia leo.
Pia Jeshi hilo limesema Barabara tisa jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.
Post a Comment