*****
Beki wa Simba, Che Malone Fondoh amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kufanya makosa yaliyoigharimu timu hiyo katika michezo miwili ya kimataifa.
Fondoh alifanya makosa hayo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Bravos ya Angola mechi iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 na Simba jana na awali wakishinda 2-1 dhidi ya CS Sfaxien kwenye Uwanja wa Mkapa.
“Napenda kuomba radhi familia nzima ya Simba kwa kuwagharimu katika mechi mbili,” ameandika katika mitandao yake ya kijamii.
“Ninawajibika kikamilifu kwa makosa yangu na kuahidi kufanya kazi kwa bidii zaidi Ili kufanya vizuri zaidi katika siku zijazo.”
Post a Comment