*******
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili
kutokana na jinsi ilivyojipanga kila siku kutoa huduma za dharura
zinazopokelewa kutoka Hospitali mbalimbali nchini, watu binafsi na wale
wanaoletwa na Jeshi la Polisi na kupata huduma kupitia Idara ya Tiba na
Magonjwa ya Dharura pamoja na Kitengo cha Dharura kwa Kina Mama Wajawazito.
Hayo
ameyasema leo alipofanya ziara Hospitalini hapo kuangalia hali ya utoaji huduma
hususani mfumo mzima wa utoaji huduma za tiba kwa wagonjwa wanaopata dharura
mbalimbali ikiwemo ajali au kuumwa ghafla na kuongeza kuwa hospitali imejipanga
vizuri na imeanza kuchukua hatua kutokana na kuwa na mfumo unaoonesha taarifa
zinavyokuja kutoka kwa wananchi, kufanyiwa kazi na wananchi kuhudumiwa na
kuahidi kuimarisha zaidi eneo hilo.
“Nawapongeza
wenzetu Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kazi kubwa mnayoifanya katika
kuhudumia wananchi, nasi tupo hapa kwenye mradi wa kuimarisha huduma za
matibabu ya dharura ambalo ni eneo muhimu kwa sababu ndiyo hasa linasaidia
kuokoa maisha inapotokea dharura ambayo inaweza kuwa ajali au ugonjwa wa ghalfa
au jambo lolote lile la kiafya” amesisitiza Dkt. Jingu.
Ameeleza
kuwa Serikali ilisambaza vifaa na magari mengi ya utoaji huduma za dharura kwa
hospitali mbalimbali nchini na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliielekeza
Wizara kuhakikisha magari yote na vifaa vilivyosambazwa vinafanya kazi
iliyokusudiwa na magari yaratibiwe kwa karibu zaidi.
Katika
ziara hiyo ya kufuatilia utekeleza wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt. Jingu amesema
kuwa ili hayo yafanyike vizuri, inabidi kuimarisha mifumo ya mawasiliano ya
kidigitali ya kufuatilia magari pamoja na vifaa vingine ili kuweza kuratibu
huduma ya magari ya wagonjwa ipasavyo na kuhakikisha vinafanya kazi wakati wote
na ipasavyo.
Aidha
aliongeza kuwa huduma za dharura hazitaishia tu kwenye magari bali pia mfumo
huo uwezeshe watoa huduma wa dharura au anayepatiwa huduma kutoa taarifa za
msingi za mgonjwa ili mgonjwa huyo anapofika hospitali apate huduma haraka
kutokana na taarifa zake kuwafikia mapema watoa huduma katika hospitali na
kuwawezesha kuwa tayari kumhudumia mara tu anapopokelewa Idara ya Tiba na Magonjwa ya Dharura inahudumia wagonjwa 150 hadi 200 ambapo kati yao 100 ni rufaa za simu kutoka hospitali mbalimbali, mtu mmoja mmoja na rufaa binafsi kutoka nyumbani ambapo kwa upande wa Kitengo cha Dharura kwa Kina Mama Wajawazito nacho kinapokea wagonjwa kati ya 20 hadi 35 kwa siku wenye uhitaji wa dharura mbalimbali.
.
Post a Comment