Tausi Mbowe, Dar
Katika kuhakikisha inatoa elimu kwa videndo Mamlaka ya Dawa ana Vifaa Tiba imekuwa ikishirikisha wanafunzi mbalimbali wakiwamo wanafunzi wa Afya nchini.
Miongoni mwa wanavyuo hao ni pamoja na Chuo cha Afya cha Paradigms College lilichopo jijini Dar es Salaam, Muhimbili na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Hivi karibuni Mammala hiyo imetoa mafunzo kwa kwa vitendo yanayohusu masuala mbalimbali ya afya.
Wanafunzi hao walipata mafunzo mwenzi Januari 025 katika ofisi za Mamlaka hiyo Kanda ya Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine wanafunzi hao wamejifunza kwa vitendo mambo mbalimbali ya Dawa, Vifaa na Vitendanishi.
Sambamba na mafunzo hayo wanafunzi hao walipata fursa ya kutembelea maabara za kisasa zilizopo katika ofisini hiyo.




Post a Comment