Lissu amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho baada ya kumshinda aliyekuwa mwenyekiti Freeman Mbowe na kuhitimisha ufalme wake wa miaka 21 katika kiti hiko.
Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile kupitia taarifa yake aliwapongeza viongozi wengine waliochaguliwa akiwamo Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche pamoja na John Mnyika aliyeteuliwa kuendelea na wadhifa wake wa Katibu Mkuu.
Aidha, TEF imempongeza mwenyekiti mstaafu, Mbowe kwa ukomavu aliouonyesha na kukubali matokeo kisha kukabidhi madaraka kwa amani jambo linaloashirikia kukua kwa demokrasia ndani ya chama hicho.
Balile alimtaka mwenyekiti huyo mpya aliyechaguliwa kuendeleza ushirikiano na vyombo vya habari ili kujenga Taifa
Post a Comment