Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekipiga marufuku kituo cha televisheni cha Al Jazeera kufuatia mahojiano yake iliyofanya na kiongozi wa kundi la waasi la M23 ambalo limeteka maeneo mashariki mwa nchi.
Kulingana na msemaji wa serikali ya Kongo, Patrick Muyaya, mamlaka ya nchi hiyo ilibatilisha kibali cha waandishi wa shirika hilo nchini humo na kwamba kituo cha Al Jazeera kilimuhoji mkuu wa mtandao wa ugaidi bila kuwa na kibali.
Siku
ya Jumatano kituo cha televisheni cha Al Jazeera kilimuhoji Bertrand Bisimwa,
Mkuu wa kundi la waasi la M23 linalopambana na jeshi mashariki mwa nchi.
Katika mahojiano hayo Bisimwa, aliishutumu serikali ya Kinshasa kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo mwezi Agosti na kudai kwamba kundi la M23 linaendesha "vita kamili vinavyoendelea."
Muyaya
aliyafananisha mahojiano hayo kuwa sawa na kuukumbatia ugaidi na kwamba hilo
halikubaliki na kuwataka wanahabari kutotoa fursa kwa magaidi.
"Niliamua,
baada ya tathmini na mashauriano na timu yangu, kuondoa vibali vilivyotolewa
kwa waandishi wa habari wa AlJazeera" Muyaya aliwaambia waandishi wa
habari.
Cc Dwkiswahili
Post a Comment