.......................
Jeshi la Polisi Kamnda Maalum ya Dar es salaam limesema Jumla ya madereva 179 wametuhumiwa na kupimwa ulevi kati yao madereva 30 walikutwa na ulevi kiwango cha zaidi ya miligramu 80 katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya 2025
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Kamanda wa Jeshi Hilo SACP Muliro Muliro amesema pia kati yao Madereva 22 walitokea Wilaya ya Kinondoni, madereva 06 Wilaya ya Ilala na madereva 02 Wilaya ya Temeke.
Kamanda Muliro amesema kuwa usimamizi wa sheria na kanuni za usalama barabarani zilisimamiwa kikamilifu ili kuweza kudhibiti ajali za barabarani.
Post a Comment