MFAHAMU ALIYEFUNGA BAO LA KWANZA EPL 2025


 ****

Bryan Mbeumo ndiye mchezaji wa kwanza kufunga bao kwa mwaka 2025 Katika ligi kuu nchini Uingereza (EPL).

Nyota huyo wa Brentford anayecheza nafasi ya ushambuliaji ameandika rekodi ya kipekee kwa ligi kuu ya Uingereza na atakumbukwa kwa ubora aliouonyesha katika mchezo dhidi ya Arsenal. 

Brentford walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Bryan Mbeumo dakika ya 13 lakini bao hilo lilisawazishwa na Gabriel Jesus dakika ya 29 na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikifungana bao 1-1.

Arsenal imekuwa na mwendelezo mzuri katika mechi 5 zilizopita ikivuna alama 11 kwa kushinda michezo mitatu mfululizo na sare mbili.

 


0/Post a Comment/Comments